Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo (Jumatano – 2 Julai, 2025) umeshuhudiwa mkusanyiko mkubwa wa Wananchi wa Iran, uliofanyika katika Mji wa Qom ili kuonyesha utayari wao katika kuyahami Matukufu ya Kiislamu, kuihami Heshima, Sharafu na Izza ya Kiislamu, kuwahami Viongozi wa Kiroho wa Kiislamu, na kwa ajili ya kuuhami Mfumo sahihi wa Uongozi wa Wilayat Al-Faqih, na kwa ajili ya kumhami Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Al-Qaid, Ayatollah Ali Khamenei (Allah Amhifadhi, na kwa ajili ya kulaani vitendo vya uchokozi vya utawala haram wa kizayuni, katika kuishambulia jamhuri ya kiislamu ya Iran, na kuwaua wananchi wasio kuwa na hatia watoto na wanawake, na kulaani shambulizi la Marekani katika vituo mbalimbali vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Tumefanikiwa kuuliza maswali mawili na kupata maoni ya waandamanaji wakijibu maswali yetu hayo mawili ya msingi ambayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Swali la Kwanza: Ushujaa huu Iran wameutoa wapi? Kwa nini watu wa Iran ni Majasiri?.
Swali la Pili: Tafadhali tuambie, je, unampenda sana Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Ayatollah Khamenei) au la?.
Sikiliza majibu ya Wananchi wa Iran katika klipu hapo juu, kuhusiana na maswali hayo mawili ya msingi.Hakika ni majibu maridhawa.
Your Comment